Geita: Wananchi wa Mtaa wa Buhalahala ,kisesa na
Moringe wamewafungia ndani waandikishaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura na kupiga mawe gari za serikali kisha
kuvunja vioo vya nyuma kwa kile kinachoelezwa kuwa muda wa kuandikishwa
umekwishana wao hawajaandikishwa.
Wananchi hao waliamua kuchukua maamuzi hayo kutokana kuhofia kutokuandikishwa na kukosa haki yao
ya msingi ya kupata kitambulisho kitakachowawezesha kumchangua kiongozi
wamtakae na pia kitambulisho hicho kuwasaidia katika mabo mbalimbali ikiwamo
kusafiri na matibabu.
Zoezi hilo ambalo lilianza 17 Juni mwaka huu kwa kata tatu
ambazo ni Buhalahala,Mwatulole na Kalangalala za mjini Geita na kumalizika 23 Juni mwaka huu(Jana) ilizua taflani katika vituo hivyo ambapo
wananchi walikaa kituoni hadi usiku huku wakizuhia waandikishaji wasiondoke
kituoni mpaka wananchi wote waandikishwe.
“Mimi nimekuja hapa nina siku ya tano leo kila nikija sipati
nafasi ya kuandikishwa,wanaadikisha watu wenye pesa zao sisi maskini tunabaki
kuangalia tu,wengine wanalala wanakesha vituoni siku ya tano lakini hawajaandikishwa
na leo ndiyo mwisho”alilalamika Marwa Ernest mkazi wa mwatulole.
“Tumemzuhia huyo anayeandikisha hasitoke ndani mpaka
atuandike wote tuliopo hapa ,hatuogopi cha polisi wala cha nani kama nikutua
watatuulia hapa ,tunachotaka ni haki yetu ya kuandikishwa ,cha kushangaza
wanaacha kutuandikisha wazawa wa eneo hili wanandikisha watu wanaotoka kata
zingine hiyo ni haki kweli?”alihoji
Neema Charles.
Charles aliongeza,”chakushangaza mwandikishaji anatuambia
macho hayaoni ,kwa hiyo sisi tufanyeje, tunataka kitambulisho kwani ndiyo cha
msingi mwaka huu”alilalamika.
Wananchi hao ambao walionekana kuwa na jazba huku wakitishia
kuchoma mashine kama hawataandikishwa
walisikika wakisema kuwa zoezi hilo lilijaa ufisadi kwani watu wengine
wenye pesa waliandikishwa kwa njia ya simu yaani watu walituma taarifa zao kwa
simu na kuandikishwa.
“Msiachie wazi huko baneni
mlango,kazeni uzi huko msimpe nafasi ya kupita mpaka tujue muafaka wetu
haiwezekani watu tunakuja kila siku hapa tukifika tunaambiwa tuandike majina
lakini hatupewi vitambulisho ,hapa hatoki mtu ...tunataka fomu...tunataka
kitambulisho”walisikika wananchi wa
buhalahala.
“Mtu yupo nyumbani
amelala anaandikishwa,sisi tuliokuja kukesha hapa tunaambiwa twende kalangalala wao wamechoka macho
yanawauma ,hivi hatima yetu nini na sasa ni saa 3:00 usiku kwanini
wasituandikishe ?hatoki mtu hapa ,kama
ni polisi aje tu”alisema Julius Maugo mkazi wa Mwatulole.
Katika kituo cha Kalangalala Sekondari hali nayo ilikuwa
tata ambampo mwananchi ilifika eneo hilo majira ya saa 1:30 na kushuhudia
wananchi zaidi ya 200 wakiwa kituoni wengine wakipigana ngumi na kusukumana
kila mmoja anataka aandikishwe.
“Hapa muda unaisha ,na leo(jana) ndiyo mwisho,hatujui hatima
yetu ,wananchi wengi hatujaandikishwa,tumeshaomba tuongezewe mashine lakini
hatusikilizwi zaidi tunashuhudia wenye pesa ndiyo wanaandikishwa”alisema
alisema Mariana Peter mkazi wa kisesa.
Hata hivyo hali ilikuwa mbaya zaidi ilipofika saa 4:00 usiku
ambapo wananchi waliamua kupiga fgari ya serikali mawe na kuvunja.
Hata hivyo kaimu mkurugenzi wa halamshauri ya mji Hellen Kahindi aliamua kuongeza muda wa zoezi hilo kwa kata amabzo hazikukamilika ikiwamo Buhalala ,Kalangalala na Mwatulole na zoezi hilo litaanza kesho kwa kata zote za mjini kwa muda wa siku saba.
tumefanikiwa kutuliza vurugu za kufungiwa ndani kwa baadhi ya waandikishaji,licha yakuwa tumepata hasara ya kuvunjwa vioo vya mbele magari ya serikali ,lakini kilio cha wananchi tumekisikia na tatahakikisha wote wanaandikishwa
0 comments:
Post a Comment