Geita:Waandishi wa habari mkoa wa Geita wametakiwa kutunza kazi zao za kihabari kwa umakini ili kuepuka kuvuja kwa taarifa zao za siri au kuibiwa kwenye mitandao.
Hayo yalisemwa jana kwenye mafunzo ya matumizi ya mitandao yaliyofathiliwa na Media Institute of Southern Africa (MISATAN) na mkufunzi wa mafunzo hayo Flora Rugashoborola, ambapo alisema kuwa katika karne hii ya utandawazi kumefumuka wimbi la kazi za waandishi kuibiwa kwenye mitandao hali inayohatarisha maisha yao.
"mwandishi wa habari unatakiwa kufahaamu jinsi ya kulinda kazi zako zisiibiwe kwenye mitandao ili kulinda usalama wako,nasema hivi nikimaanisha kuwa kutokana na utandawazi kukua kumekuwa na wimbi la wizi wa kazi za watu kwenye mitandao"Rugashoborola.
Alisema "kwasasa watu wanaingia kwenye mitandao,mfano kwenye email zenu mnazotumia kutuma stori zenu na kuangalia habari zako unazotuma ,yawezekana unaandika habari za uchunguzi zinazogusa maslai ya mtu na wewe hutaki kujulikana kama unaandioka habari hizo inaweza ikatoke mtu akafatilia na kubaini wewe ndiyo unaandika"alisema
Aliweka bayana kuwa ili kujikinga na madhala hayo ni wajibu wa mwandishi kubadilisha neno la sili analolitumia kwenye mitandao mara kwa mara,pia kweny vifaa vyake mfano komputa anatakiwa kuweka neno la siri kwenye kila kablasha au kapu analolitumia kutunza andiko lake kwenye komputa.
"msiache ovyo kompyuta zenu,msimwazime mtu usiye na imani nae na hata kama unamwamini usimwamini kwa kazi zako za siri,tunza kazi zako za siri sehemu ambayo mtu wa kawaida hawezi kuona "alisema.
Aidha baadhi ya waandishi waliohudhulia mafunzo hayo walisema tatizo la wizi wa kazi zao lipo ila walikuwa hawajajua jinsi ya kujikinga na hilo,kwamba kuna wengine walishaingia kwenye hatari ya mtu kuingia kwenye mtamdao wa Emaili na kuchapa habari ya uongo kisha kuituma ofisini anakofanyia kazi .
"iliwahi kutokea mimi sijui chochote ,kumbe kuna mtu kaingia kwenye email yangu akachapa taarifa akaituma ofisini na hiyo habari ikatoka kwenye gazeti ,taarifa hiyo ilinipa shida kwani haikuwa na ukweli hata chembe"alieleza hayo Vallence Robart.
Hata hivyo waliishukuru MISATAN kwa kuandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa Geita na kwamba yamewafungua akili ya kufanya kazi zao kwa usalama zaidi.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment