WATOTO ,WANAWAKE WAJAWAZITO WALIVYO HATARINI KUATHIRIKA NA SUMU YA ZEBAKI



Jackline Masinde
Geita:Ilikuwa ni dakika 45 ya saa 4:00 asubuhi tangu nilipofunga safari  kukifikia kijiji cha Nyakabale kilichopo mjini Geita.

Nikiwa kijijini hapo, niliona  nyumba nyingi zilizojengwa mithili ya makambi ya wakimbizi ama mahema.

 Wakazi wa eneo hilo walionekana wakichapa kazi haswa.


Magari yalipishana,pikipiki nazo hazikuwa nyumba ambazo zilionekana zimebeba viroba vya mawe na abiria wanneau zaidi  kwenye pikipiki moja maarufu kama mishikaki.

Hakika watu wa kijiji hiki hawakuwa wavivu haslani kwani kila mtu alijishughulisha,si watoto,si vijana,si wanaume wala wanawake.

Laiti kama watu wote nchini wangekuwa wanafanya kazi kama wanakijiji hawa hakika Taifa lingekuwa mbali kimaendeleo.

Walionekana wakibeba mawe,wengine wakianika udongo,wengine wakiponda mawe,wengine wakifua dhahabu kwenye makarai na magunia.

 “Lete mawe wewe acha kuzubaa,hali ya hewa inabadilika, mvua muda wowote inanyesha”alisikika kijana mmoja.

Pia nilishuhudia makundi ya vijana yakiwa yamebeba nyundo,sururu na Moko wengine walipanda na wengine walishuka toka milimani.

“Hoya wahi mida ya mafeed kunywa Chai”alisikika mmmoja wa vijana Kijijini hapo.

Kweli kijiji hiki kilichangamka sana,ukiachilia mbali pilika nilizoziona pia  nilisikia kelele za mashine zikisaga mawe.

Ilikuwa ni kelele ya aina yake ,kusikilizana ilikuwa shida kwangu,lakini wao walionekana kuzoea hali hiyo.

Ukiachilia mbali kelele za makarasha pia kulipigwa mziki wa juu kwenye baa zilizopo kijijini hapo.

Ilikuwa ni kazi mtindo mmoja lakini na starehe pia kwani wengine walifanya kazi na wengine walionekana wakinywa pombe asubuhi na mapema.

“Wewe mama ongeza bia moja,hapa ni starehe na kazi mtindo mmoja ..leta tukushikie mtoto huyo,mtakujaje na watoto kazini?”alisikika kijana mmoja akimhoji binti wa miaka 18 aliyekuwa akiwahudumia.

Zaidi niliona wanawake wengi.Wengine wajawazito,wengine wakinyonyesha watoto na wengine wakiwa wamepakata watoto wao wachanga migongoni, huku wakigoroga udongo uliyochanganywa na maji kwa kutumia mikono yao kwenye makarai.

Baadae niligundua kuwa matope hayo ni udongo unaosadikiwa kuwa na dhahabu,iliyochanganywa na sumu ya zebaki ,ulikuwa ukisafishwa tayari kwa kupata dhahabu.

Pia nilishuhudia Watoto wadogo kuanzia 0-5 walikuwa wakicheza chini michezo ya kitoto.Walijipikilisha kwenye makopo na wengine wakiwaigilizia wanavyofanya mama zao kwa kukoroga udongo kwenye makopo.

“Nipe kopo langu...mama niwekee udongo na mimi nikoroge”alisikika mtoto wa umri wa mika 5 akimweleza mama yake mzazi.

Watoto wengine walikuwa wakicheza mpira,wengine walikuwa wakichezea maji machafu ambayo yalionekana yakitililika kutoka kwenye mwalo wa kusafisha dhahabu.

Maji hayo niyale ambayo tayari yamechanganywa na sumu ya zebaki ambayo nihatari kwa afya ya mwanadamu.

Aidha niliona watoto wengine wakikoroga udongo kwenye makarai.Watoto hao walisadikika kuwa na umri wa miaka 6-15.

Wengine walikuwa wakizurula ndani ya machimbo hayo wakisubiri kupewa vibarua vya kusafisha dhahabu,huku wasichana wadogo wengine wakiwa wameketi katika baa wakisubiri wateja.

Ilinipa wakati mgumu sana kujua kwanini kijiji hicho kina wanawake wengi na watoto wadogo ambao wanafanya kazi ya uchimbaji jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi na sera ya mtoto

Wakati nikiwa bado ninatafakari hayo mara nilimuona mama mmoja mwenye miraba mine,amabye baadae aliniambaia ana umri wa miaka 35.

Mama huyo ulikuwa akifanya kazi ya kukoroga udongo kwenye makarai aliwakati huo akiwa amezungukwa na watoto wake wanne.

Nilimsogelea mama huyo na kuomba kuongea nae ambapo mazungumzo yetu yalianza hivi:

Mwandishi:pole mama na kazi..

Mama:Asante mwangu ,karibu(alinikalibisha)
Mwandishi: Asante mama,kwanza Shikamoo..
Mama ;Marahaba mwanangu.

Niliketi kwenye ndoo iliyokuwa jirani na mama huyo.

Mwandishi:samahani mama(nilijitambulisha).

Mama:Nashukuru kukufahamau mwanngu,wengine sisi tulishazoea shida tu kama unavyotuona tunahangaika na makarai haya..

Kauli ya mama huyo ilinivuta na kutaka kufahamu zaidi.

Alijitambulisha kuwa yeye ni Kabula Satongima (35)ni mama mjane mwenye watoto wanane.

“Nilizaliwa kijiji cha Bupandwa wilaya ya Sengerema mkoa wa mwanza,ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 15  katika tumbo la mama na baba yangu”alijitambulisha.

 Satongoma alisema kuwa aliolewa akiwa na umri wa mika 14 huko kijiji cha Nyiboko Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara.

“Niliishi na mume wangu huko Nyiboko maisha yakawa magumu mwaka 2013 mwazi januari mume wangu alihamia Geita ikiwa nimoja ya kutafuta maisha”alisema mama huyo.

Satongima alieleza kuwa  aliamua kumfata mume wake na kuja kuishi nae katika kijiji cha Nyakabale.

Nikiwa nyakabale nilipata ujauzito wa mtoto wangu wa mwisho,lakini wakati naendelea kulea mimba yangu mume wangu alikuwa akifanya kazi ya kuokota mawe yanayotupwa na wazungu”alisimulia.

Alisema siku moja mume wangu aliondoka nyumbani alfajiri na kwenda msituni kutafuta mawe,akiwa huko alipigwa risasi na askari wa fanya fujo uone(FFU) akafariki dunia.

Nililetewa tu taarifa na wenzake,hivi ninavyoongea hata maiti ya mume wangu sikuiona na sijui alizikwa wapi”alisema .

Mama huyo alisema “mama humu unavyotuona wanawake wengi waume zetu wamekufa kwa kupigwa risasi na askari wanaolinda mgodi”alisema.

Hakika mama huyu alionekana kutokujua chochote juu ya haki za watoto na ulinzi kwa mtoto,na wala halionekana kutojua kama kumtumikisha mtoto kazi ni kosa kisheria.

“Dada hizo sheria mimi sizijui...sijasoma,ninawatoto wengi wasiponisaidia kazi tutakula nini?na sinauwezo wakusema niwasomeshe”alilalamika kwa kujitetea.

Nilimuuliza mama juu ya kazi yake ya kuosha dhahabu kuwa ana muda gani anafanya kazi hiyo na amenufaika nanini.

“Mama hii kazi tunafanya tu,lakini hakuna tunachokipata zaidi tunaambulia magonjwa tu”alisema mama huyo.

Alisema tangu aanze kufanya hiyo kazi anamiaka minne,zaidi hakuna alichonufaika nacho juu ya hiyo kazi.

“Hapa inanisaidia tu kupata pesa za kuhudumia wanagu wapate chakula basi lakini kusema iniinue kiuchumi hakuna kabisa”alisema.

Alisema kila siku asubuhi udamka yeye na watoto wake nakwenda kwenye mialo ya kusafisha dhahabu .

Hii ndiyo kazi yangu ya kila siku ,nikiamka asubuhi huwa ninawakusanya watoto wangu weote tunakuja kufanya hii kazi”alisema Satongima.

“Tukifika hapa huwa tunatafuta vibarua vya kuosha dhahabu mimi na wanangu,nikishapata huwa nawapangia wanangu karai kila mmoja anatakiwa kuosha karai 4 kwa siku”alisema.

Alisema kuwa kila karai moja analipwa sh.250 hivyo kwa siku anaweza kupata sh30,000.

Santongima aliongea yote hayo huku akiwa amezungukwa na watoto wake wadogo sana kiumri ambao pia walisafisha dhahabu iliyowekewa sumu ya zebaki.

Huwa tunakuja na mama anatuambia tuoshe dhahabu ,nasisi tunafanya ili tumsaidie mama alisema Anna Otieno (8).

Tunafanya tu,licha yakuwa tunaumia sana kukaa chini muda mrefu,pia baridi kali ikifika jioni na kichwa kinauma”alisema Otieno.

Lakini swali je mama huyu na watoto wake wanafahamu madhara ya sumu hiyo?

Mimi sijui kama inamadhara japo nasikia watu wanasema inamadahara lakini sina jinsi nikiacha kwa kuhofia madhara nitakula nini na wanangu?alihoji Satongima.

Siyo mama huyu tu aliyeonekana akifanya kazi hiyo huku akiwa na watoto wake wadogo ,lakini pia nilikutana na mama mwingine.

Naitwa Savera Jonh (20) ninamiezi sita tangu nianze hii kazi”alisema.

Nilikutana na Savera akiwa amebeba mtoto wake mchanga mgongoni aliwakati akisafisha dhahabu.

Alinieleza huku akiendelea na kazi yake kuwa alipewa mimba na kijna mmoja mchimbaji,lakini gafla mume wake huyo alipotea,hajui kama yu hai au alishakufa.

Sina kazi yakunisaidia kupata chakula na mavazi,nalazimika kufanya kazi hii”alisema Savera huku akiwekewa sumu ya Zebaki kwenye karai alizokuwa akizikoroga.

Wananwake wengi na watoto wanajihusisha na kazi ya kusafisha dhahabu bila kunzingatia usalama wao.

Nikiwa kijijini hapo nakutana na mwanamke mjamzito ambae alikuja kwenye mwalo wa Shija Boniphace akiomba kibarua cha kusafisha dhahabu.

Kaka nimekuja leo vipi kazi ipo?alihoji na kujibiwa,”kazi ipo niwewe tu kaaa tukuchanganyie udongo”alisema .

Boniphace alichukua udongo unaudhaniwa kuwa na dhahabu kwenye karai kisha kuweka sumu ya zebaki na majivu.

Pia aliweka maji ndani ya karai hilo na kumwambia mama huyo mjamzito huku akiwa amebeba mtoto wake mchanga mgongoni.

“Ninamimba ya miezi saba, mwanagu ana mwaka mmoja,nafanya vibarua ili nipate ela ya kula sina mume kama unavyoniona”alisema dada huyo.

Hakika ni huruma kwa mama huyo ambae alifanya kazi ya hatari huku akiwa amekaa chini na wakati ni mjamzito na mtoto mgongoni.

Tunaporejea katika sera ya mtoto ya mwaka 2009 inazungumzia ulinzi wa mtoto kuwa unaanzia tangu siku ya kwanza mimba inapotungwa,hivyo mama mjamzito haitaji kelele zozote ,anahitaji utulivu wakutosha ili kulinda usalama wa mtoto..

Lakini hali iko tofauti kwa mama huyo,ambae anafanya kazi kwenye makelele na sehemu ya hatari kwa mtoto aliyemgongoni na aliyekotumboni

“Siwezi kumwacha mtoto nyumbani peke yake nalazimika kuja nae huku kwasababu bado nimdogo”alisema .

Lakini mama huyu anafahamu madhara ya sumu hiyo licha yakuwa anaishika na kuitumia kila siku?
Mimi sijui kama kuna madhara,ila kila siku jioni huwa nasikia kama moto unawake kwenye mikono,kichwa kinauma na pia huwa ninababuka ngozi”alisema.

Kwa mujibu wa daktari wa hospitali ya wilaya ya Geita  Adamu Sijaona anabainisha wazi madhara ya sumu hiyo endapo mtu ataishika kula au kuvuta hewa yake.

“Zebaki ni sumu hatari sana kwenye mwili wa mwanadamu hasa inapotumika muda mrefu kwa kuigusa,kula au kunusa”alisema.

Alisema moja ya madhara makubwa ya sumu hiyo ni kubabuka ngozi,ngozi kupasuka ,ngozi kuvimba na kutoa magamba,kuharibika kwa ini na inaweza pelekea kifo.

Alisema sumu huyo inamwingia mtu kupitia damu,ambapo inaenda kuathiri mfumo wa damu.

Lakini Pamoja na madhara hayo mwananchi ilishuhudia akina mama wajawazito na hata wanaonyonyesha na watoto wakiishika sumu hiyo bila hata kuwa na vifaa vya kuzuhia ngozi ya mwili kugusa sumu hiyo.

Watoto wadogo akiwamo Tereza Jonh (14) na Hapness Deusi (13) walionekana wakimiminiwa sumu hiyo kwenye karai lililokuwa na udongo unaodhaniwa kuwa na dhahabu,kisha waliishika sumu hiyo wakati wakichanganya sumu na udongo kwa mikono yao.

Watoto hawa wanaishi mbali na wazazi wao kwani Tereza wazazi wake wako katoro lakini yeye yuko Nyakabale kwenye machimbo.

“Huwa nalala huku kila siku kwa rafiki zangu,asubuhi kukicha tunazunguka kutafuta vibarua humu machimboni”alisema Tereza.

Anasema usalama wake ni mdogo sana kwani kunasiku zingine wanabakwa na wachimbaji,siku zingine wakikosa vibarua wachimbaji wanawaambia wakafanye nao tendo la ngono ndiyo wawaepe vibarua.

“Niliwahi kubakwa na mchimbaji,niliomba ela ya kula kwa mchimbaji Yona ,jioni ilipofika akaniambia nimlipe...nikakataa ndipo aliponibaka mbele ya wenzangu”alisema.

 Pia mama mjamzito Naomi Gerald (18) mwenye ujauzito wa miezi 5 alionekana akimiminiwa sumu hiyo kwenye karai lillilokuwa na udongo na maji .
 Dk Sijaona alibainisha pia madhara ya sumu hiyo kwa watoto wachanga wanaonyonyeshwa,wanawake wajawazito na watoto wadogo.

Alisema mtoto mchanga anayenyonyeshwa anapoigusa sumu hiyo,au kuila anaweza kuwa na midomo myekundu,nywele kunyonyoka,,kudhohofika kwa mwili kupoteza uwezo wa kuona kwenye mwanga,inaathiri pia ukuaji wa mtoto.


Hii sumu ni hatari pia kwa watoto wachanga,wanaweza ipata kupitia maziwa ya mama ambae ameathirika na sumu hiyo,pia mtoto anapoigusa “alisema Sijaona

Alisema kwa upande wa mama mjamzito,anaweza kuzaa mtoto njiti,kuzaa mtoto akiwa na upungufu wa uzito,mimba kuharibika,au kuzaa mtoto mwenye kasoro ya viungo vya mwili.

“mama anaweza kupata shinikizo la moyo,kupooza ,kupata magonjwa ya figo,kuumwa na kichwa sana  na kuwa na baridi kali”alisema.

Sofia Elias ni moja ya wananwake anaeleza kupata madhara ya ngozi ya mwili wake baada ya kuanza kufanya kazi hiyo alianza kuvimba ngozi yake .
“ilitokea tu baada ya kufanya kazi hii ya makarai nilianza kuvimba miguu na mikono na baadae ilianza kubabuka ngozi”alisema.

“Niliacha kwa muda kazi hiyo hali ikarudi kuwa nzuri,lakini nimelazimka kurudia kazi hii ili kujikwamua na umskini.

Elina Masanja nimama mwenye watoto wawili,anaeleza kuwa huwa anakuja na watoto wake hao kufanya kazi ya kuzungusha.

Mwanangu kama unavyomuona hali yake ya afya siyo nzuri,huwa anaumwa mara kwa mara,afya yake nidhohofu sana nywele zake zinakuwa nyekundu”alisema.

Kwa mujibu wa Dk sijaona anasema kuna kesi mbalimbali za magonjwa yanayoshabiana na madhara ya sumu hiyo lakini hawana uthibitisho sahii juu ya ugonjwa huo kama chanzo chake ni sumu ya zebaki.

“Katika hospitali yetu ya wilaya tunapokea kesi za mimba kuharibika 8,9 hadi 10 kwa mwezi ,pia wagonjwa wenye matatizo ya ngozi ni 5-6 kwa mwezi huku kwa upande wa watoto njiti ni 2-3 kwa mwezi”alisema.

Kutokana na takwimu za Mganga huyo tunaweza sema kwa mwaka zaidi ya mimba 120uharibika,huku watu wenye matatizo ya ngozi ni zaidi ya 36 mwaka.

Lakini wanaowapa vibarua hawa akina mama na watoto wanasemaje juu ya usalama wao?
Shija Boniphace ni mmoja wa wamiliki wa mialo machimboni hapo.

Alisema madhara wanayafahamu lakini wengi walikuja wakiliia kufanya hii kazi na hatuwezi kuwazuia.

Wasipofanya kazi watakula nini dada?sisi hapa ni wachimbaji wadogo hatuna uwezo wa kununua vifaa vya kuwapa hawa akina mama na watoto pindi wanapofanya kazi ya kusafisha Dhahabu”alisema mmiliki huyo.

Naamini sheria zinazomlinda mtoto zipo katika ofisi zote hapa nchini,swali langu hizi sheria zimewekwa kama mampambo au la...Pia mkoa wa Geita unamashirika zaidi ya 50 yanajihusisha na mabo ya haki za watoto,lakini suala la ajira hatarishi na usalama wa mtoto bado nikubwa na kila siku kunamashirika yanapewa misaada.


Uongozi wa kijiji unasemaje?.

Deusi Zabron ni Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Nyakabale anakili kuwepo kwa wanawake na watoto wanafanya kazi hatarishi ya kuchenjua dhahabu bila kuzingatia usalama.

Ufanyaji wa kazi kwa watoto wadogo kazi za madini na wanawake wajawazito ni kinyume cha sera ya madini ya mwaka 2010 inayozuhia watoto wadogo kuwepo katika maeneo ya migodi.

Pia sera hii inazuhia watoto kujihusisha na kazi yoyote ndani ya machimbo ama migodi lakini kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi ya mtendaji zaidi ya watoto 2000 wanajihusisha na kazi za uchimbaji kijijini hapo.

Tumeweka sheria kwa wamiliki wa migodi,zinazozuhia watoto na wananwake kutoenda na watoto maeneo ya machimbo lakini inaonekana kuwa ngumu kwani tunazuhia lakini wanakwenda”alisema.

Alisema wanawake waliowengi na watoto wanategemea kazi za madini kuendesha maisha yao sasa unapowazuhia wanakuona kama mbaya kwako.

“tunaamua tu kuwaachia wakati mwingine,maana tunazuhia lakini watoto wengi unawakuta ,wanatumwa na wazazi wengine,wengine wanakuja na wazazi wao,wanakwambia hawana wakuwaachia”alisema.

Hata hivyo mwananchi ilimfata ofisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita Pius Lobe kuzungumzia hali hiyo ,alishindwa kutoa ushirikiano huku akihitaji barua kutoka kwa mwandishi ya kuomba kibali kutoka ofisi yake yakupewa taarifa.

Mimi ninataratibu zangu kwenye ofisi napata utitili wa waandishi wengine ni makanjana,hivyo nakuomba uandike barua ya kuomba hizo taarifa”alisema.

Hata hivyo barua hiyo iliandikwa,lakini mpaka sasa haijajibiwa ,na hata nilipofatilia nilijibiwa na mmoja wa wafanyakazi katika ofisi hiyo kuwa niende ngazi nyingine ili kupata maelezo kwani ofisa huyo yuko na kazi nyingi

Shirika la plan Itanational ni moja ya Shirika kubwa hapa nchini ambalo limesambaa karibia mikoa mingi hapa nchini .

Shirika hili likifunga mradi wake wa kutokomeza ajira hatarishi kwa watoto wilaya ya Geita na Nyang’hwale hivi karibuni linabainishawazi suala la watoto kufanya kazi hatarishi migodnini.

“Tulifanya utafiti mwaka2012 tukabaini zaidi ya watoto12,500 wako katika ajira hatarishi,ndipo tukaanza kazi ya kusaidia kuondoa tataizo hilo “alisema meneja wa miradi ya kutokomeza ajira hatarishi kutoka shirika hilo.

Alisema baada ya kuanzisha kampeni ya kutokomeza ajira hatarishi kwa watoto maeneo ya migodini walisaidia kuwaondoa watoto 12,036 ambapo kati ya hao 6502 wamerudishwa shule.

Alisema kampeni hiyo ilihusisha vijiji 52 vilivyopo ndani ya wilaya mbili ya Nyan’ghwale na Geita.

Pamoja na kampeni hiyo ambayo haijasambaa maeneo yote ya Geita,bado kunauhitaji mkubwa wa kufanya kampeni za namna hiyo kwa wingi katika kijiji cha nyakabale ili kuokoa lundo la watoto ambao wanaishi katika mazingira hatarishi ya kufanya kazi ambazo ni hatari kwa afya zao.

Pia jamii bado inahitaji elimu ya kutosha  juu ya usalama wa mtoto na matumizi ya sumu ya zebaki,haki za watoto tangu akiwa tumboni  hadi miaka 18.

Umaskini katika eneo hili ndiyo changamoto kubwa kwa wananchi wengi  hususana kwa akina mama,wanawake waliopo maeneo hayo wapewe mikopo na kufundishwa ujasiliamali.

Serikali ishiriki kwa kina kusimamia sheria zilizowekwa,wahusika wafanye kazi  wasiishie kukaa katika maofisi yao na kusubiri mashirika binasfi ndiyo wafanye kazi hizo.

Wananwake na watoto wao wakifanya kazi ya kuchenjua dhahabu kwenye makarasi


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment